2721; Kazi na bei.

Siku za karibuni nimekutana na nukuu inayohusu kazi na bei ambayo imenifikirisha sana.

Nukuu hiyo kutoka kwa asiyejulikana inasema; “Kama unataka kununua vitu bila kuangalia bei, unapaswa kufanya kazi bila kuangalia saa.”

“If you want to buy things without looking at the price, you need to work without looking at the clock.” –Unknown

Hebu isome tena tararibu ili inase kwenye akili yako kwa uhakika.

Tukiichimba nukuu hiyo kidogo, imebeba maana kubwa.
Kwamba kama unataka bei za vitu zisiwe kikwazo kwako, basi muda wa kazi haupaswi kuwa tatizo kwako.

Kwamba ukiweka muda wako wote kwenye kazi, utaweza kumudu chochote unachotaka.

Na hilo lipo wazi kabisa.
Masikini, ambao hawawezi kumudu vitu vingi kwenye maisha yao, huwa wanafanya kazi wakiangalia muda.
Muda wa kazi ukiisha huwa wanafurahia na kuondoka mara moja au kufunga biashara zao haraka.
Halafu wanaenda kutumia muda ambao hawafanyi kazi kufanya mambo ambao ni ya hovyo.

Matajiri, ambao wanaweza kumudu chochote wanachotaka, huwa wanafanya kazi bila kuangalia muda.
Kama kuna kitu wanataka kukifanya, watakifanya mpaka wakikamilishe bila kujali ni muda kiasi gani inawachukua.
Na hilo ndiyo linawafanya wazidi kupata fedha zaidi.

Tukiendelea kuichimba kauli hiyo zaidi tunaendelea kuona kwamba matajiri, pamoja na kuweza kumudu chochote wanachotaka, bado wanaweka muda wao mwingi kwenye kazi kuliko kutumia fedha walizonazo.

Lakini masikini akipata pesa kidogo tu yupo tayari hata kutukana kazi au biashara yake, akiiona ni kitu kisichokuwa na maana yoyote kwake.
Atatumia muda mwingi kwenye kutumia fedha kidogo aliyonayo kuliko kufanya kazi zaidi.
Na hilo ndiyo linapelekea masikini kutenganishea haraka sana na fedha zao.

Hatua ya kuchukua;
Fanya kazi bila kuangalia muda ili uweze kununua vitu bila kuangalia gharama.
Kadiri unavyopata fedha, ndivyo unavyopaswa kuweka muda zaidi kwenye kazi kuliko kwenye kuzitumia fedha hizo.

Tafakari;
Masikini wanaouonja utajiri kidogo huwa wanarudi haraka kwenye umasikini wao kwa sababu huwa wanaweka muda mwingi kwenye kutumia fedha zao kuliko kuweka muda kwenye kuzizalisha zaidi.
Epuka njia hiyo ya uhakika ya kubaki kwenye umasikini, muda wa kutafuta fedha unapaswa kuwa mwingi kuliko muda wa kuzitumia.

#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining