#SheriaYaLeo (225/366); Tumia hisia zao.

Kama unataka kumshawishi mtu abadilike, usipingane na hisia zake, bali zitumie hizo kuchochea mabadiliko.

Kama mtu ni mkorofi na mtukutu, badala ya kuyapinga hayo, mweke kwenye hali ya kutaka kubadilika ili kuonyesha ukorofi na utukutu wake.

Kwa kuyafanya mabadiliko yaendane na kile ambacho tayari mtu ana sifa nacho, atabadilika ili aendelee kutunza sifa ambayo ameshajijengea.

Hata kama ni sifa ya kijinga na isiyo na maana, mtu atasukumwa kuitunza kwa kila namna.

Jua kile ambacho mtu anakitaka sana na kiunganishe na mabadiliko unayotaka afanye.
Hilo litamsukuma zaidi kubadilika ili kupata kile anachotaka au kutunza sifa ambayo amekuwa nayo.

Wakati mwingine kuibua hasira ndani ya mtu kunamsukuma afanye kitu kuliko akiwa hana hasira.
Hali ya mashindano pia huwa ina nguvu kubwa kwenye kuwashawishi watu kuchukua hatua fulani.

Angalia ni hisia zipi ambazo mtu anazo, kisha zitumie hizo hizo kumshawishi kwenye kile unachotaka afanye.

Sheria ya leo; Usitumie nguvu kubwa kupinga hisia za watu, badala yake angalia jinsi ya kutumia hisia hizo kuchochea ushawishi ambao unataka kuwa nao kwao. Hisia huwa zina nguvu kubwa kwa mtu, zijue na uzitumie vizuri.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji