2724; Siyo kuanza, bali mwendelezo.

Ingekuwa kuanza kitu ndiyo mafanikio, kila mtu angekuwa amefanikiwa.

Maana karibu kila mtu alishaanza kitu fulani kwenye maisha yake.

Na watu wengi huwa na shauku na hamasa kubwa pale wanapoanza.

Lakini haichukui muda mrefu shauku na hamasa hiyo vinayeyuka na wanakosa msukumo wa kuendelea.

Huwezi kufika kwenye mafanikio makubwa kwa kuwa mtu wa kuanza na kuacha.

Unayapata mafanikio kwa kuanza na kukaa kwenye kitu kwa muda mrefu bila kukata tamaa.

Mambo mazuri mara zote huenda kwa wale wanaokaa kwenye kitu kwa muda mrefu.

Lakini hilo linachosha, kuna vikwazo na changamoto nyingi kwenye kukifanya kitu.

Kama kweli unataka kukaa kwenye kitu kwa muda mrefu, lazima ujitoe kweli kweli na usikubali chochote kikurudishe nyuma.

Hatua za kuchukua;
Hicho unachofanya sasa umekifanya kwa muda gani sasa?
Fanya maamuzi kwamba utaendelea kukifanya kitu hicho kwa muda mrefu bila kuishia njiani.
Hivyo ndivyo unavyoweza kujihakikishia mafanikio.

Tafakari;
Kiashiria cha haraka cha mtu ambaye kamwe hawezi kufanikiwa ni kuanza na kuacha mambo mengi.
Kama mtu kila wakati anaanza mambo mapya na kuishia njiani, hawezi kujenga mafanikio makubwa.
Achana na mchezo wa kuanza na kuacha.
Weka juhudi kwenye kitu kimoja na kwa muda mrefu.

#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining