#SheriaYaLeo (228/366); Tumia maigizo na siyo maneno.

Kutumia maneno kuwashawishi watu ni jambo hatari sana.
Kwani watu huishia kuelewa kinyume na kile ambacho tumemaanisha.

Maneno huwa yana nafasi kubwa ya kueleweka vibaya.
Lakini pia maneno huwa ni rahisi kuwaumiza watu na kuleta hali ya kutokuelewana.

Lakini maigizo huwa yanaeleweka moja kwa moja bila ya kuleta mkanganyiko wowote.
Maigizo yanakwenda moja kwa moja kwenye taswira na kueleweka kama yalivyoonekana.
Maigizo yananasa hisia na hivyo kuwa na ushawishi mkubwa.

Kama unataka kuwashawishi watu, usihangaike sana na maneno, badala yake tumia maigizo.
Tengeneza picha kubwa kwenye fikra za watu na wataelewa na kuvutiwa na hilo.

Sheria ya leo; Tumia maigizo kwa wale unaotaka kuwashawishi kwa kutengeneza alama na picha ambazo zinagusa hisia na kueleweka haraka. Watu wanashawishika haraka kwa kile wanachoona kuliko kile wanachosikia.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji