#SheriaYaLeo (231/360); Tumia hisia kueleweka.

Unapotumia maneno pekee kuelezea kitu, inakuwa vigumu kueleweka.
Na pia unaishia kuibua ubishi ndani ya watu ambao hawatakubaliana na maelezo yako kirahisi.

Lakini ukitumia hisia ambazo zinawanasa wengine, wanakuelewa kwa urahisi zaidi bila hata ya kuleta ubishi.

Kwa kuwafanya watu wajisikie vile unavyojisikia wewe, unakuwa umefikisha hoja yako kwa namna ambayo inapenya ndani ya watu kabisa.

Waweke watu kwenye hisia ambazo zinawafanya waelewe kwa kina kile unachowaeleza.

Fanya hilo kwa maigizo, vitendo au mfano, vitu ambavyo vina ushawishi mkubwa zaidi.

Sheria ya leo; Lengo lako linapaswa kuwa ni kuwafanya watu wapate hisia zinazowafanya waelewe kile unachomaanisha. Maneno matupu pekee hayana ushawishi mkubwa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji