#SheriaYaLeo (236/366); Jua na tumia udhaifu wa watu.
Sisi binadamu huwa tuna upinzani.
Huwa hatupendi kupangiwa nini tufanye na nini tusifanye.
Tunapenda kuona tukifanya maamuzi yetu wenyewe.
Huwa tunapinga na kukataa mabadiliko yoyote tunayopendekezewa na wengine.
Katika kuwashawishi watu, kukabiliana nao kwenye upinzani wao huwa siyo njia sahihi.
Utatumia nguvu nyingi lakini bado watabaki na msimamo wao, hutaweza kuwashawishi.
Kitu muhimu sana unachopaswa kujua ni kila mtu ana udhaifu ndani yake.
Kila mtu kuna kitu ambacho hawezi kukipinga.
Kwa kujua udhaifu ambao mtu anao na ukautumia, utakuwa na ushawishi mkubwa kwake.
Kwenye udhaifu alionao mtu, hawezi kupinga kile anachopendekezewa.
Inakuwa vigumu kwake kukataa na kupinga, kwa sababu ni kitu kinachokuwa kimemgusa kwa ndani.
Wajibu wako mkubwa ni kujua udhaifu wa unayetaka kumshawishi uko wapi.
Baadhi ya watu huonyesha udhaifu wao waziwazi.
Lakini wengine huwa wanaficha sana udhaifu wao, na hawa ndiyo huwa rahisi sana kuwashawishi ukishajua udhaifu wao.
Sheria ya leo; Kila mtu ana udhaifu, uwazi kwenye ukuta wa ulinzi waliojijengea. Ukishajua udhaifu wa mtu ni rahisi sana kuutumia kwa manufaa yako. Ni rahisi kuvuka mapingamizi ya mtu na kumshawishi kupitia madhaifu yake.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji