2735; Maana halisi ya kufokasi.

Steve Jobs aliwahi kutoa hotuba iliyopendwa na wengi sana ambapo alieleza kwa ufupi sana kwamba maana halisi ya kufokasi ni kusema HAPANA.

Haijalishi unafanya nini, kila mara utakuwa na machaguo mengi mbele yako.
Kila mara kuna vitu vizuri vitakuja.
Kuna fursa ambazo utaona hazipaswi kukupita.

Kwa kila unachosema ndiyo, tambua kinakuondoa kwenye kile kikubwa unachotaka.

Kwa maneno mengine, vitu unavyoona ni vizuri na fursa ambazo hupaswi kukosa, vinaishia kuwa usumbufu unaokuondoa kwenye kile kikuu unachotaka.

Ndiyo maana unapaswa kusema HAPANA kwa mambo yanayoonekana mazuri na fursa za kipekee.
Unapaswa kuwa tayari kukosa manufaa ya muda mfupi ili uweze kupata yale makubwa ya muda mrefu.

Kama huwezi kusema hapana kwenye fursa zinazoonekana nzuri na kuja kwako kila wakati, huwezi kufokasi kwenye kile ulichochagua mpaka kikakupa matokeo mazuri.

Kufokasi ni kusema NDIYO kwenye kitu kimoja au vichache na kusema HAPANA kwenye vitu vingine vyote ambavyo haviendani na kile ulichochagua.

Hatua ya kuchukua;
Jikumbushe kile kikuu au vichache ulivyosema ndiyo kisha kuwa tayari kusema hapana kwenye vingine vyote visivyoendana na hayo uliyochagua.

Tafakari;
Kufokasi maana yake ni kusema HAPANA kwa mambo mazuri, ili kuweka umakini kwenye yake ambayo ni bora zaidi.
Kinachowashinda wengi ni tamaa ya kutaka kupata kila kitu.
Ili upate yaliyo bora, lazima uwe tayari kukosa yaliyo mazuri.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAlGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed