#SheriaYaLeo (239/366); Tumia ndoto kubwa ambazo hawajazifikia.

Watu wengi huwa wanaamini wana uwezo mkubwa ndani yao kuliko ule unaoonekana kwa nje.

Kila mtu ana ndoto kubwa sana ambazo bado hajazifikia.
Inaweza kuwa ni mafanikio makubwa wanayotaka kufikia na ngazi za juu zaidi wanazotaka kupanda.

Bado wanakuwa hawajafika kule wanakotaka kufika kwa sababu dunia imewawia ngumu na kuwanyima nafasi ya kustawi kwa namna wanavyotaka.

Huo ni ufunguo mzuri sana unaoweza kuutumia kuwashawishi.
Kwa kuongelea ndoto zal kubwa walizonazo ambazo bado hawajazifikia, watavutiwa kukufuatilia zaidi na kushawishika na wewe.

Usiongelee tu pale watu walipo sasa, ambapo wengi hawapapendi.
Badala yake ongelea kule watu wanataka kufika, ambapo ni bora zaidi na wanapapenda zaidi.
Kwa kuongelea kile wanachopenda, wanashawishika zaidi.

Sheria ya leo; Wafanye watu wajione wakiwa juu na wakifikia ndoto kubwa walizonazo. Kwa njia hiyo watashawishika zaidi na wewe. Kwa kuzungumzia ndoto kubwa walizonazo, unawafanya wajisikie vizuri na kushawishika kwa urahisi.

#NidhamuUadilifuKujifuma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji