2737; Hakuna ambacho umewahi kufanya mara moja ukawa umemaliza.
Unakula chakula kila siku,
Hakuna kitu unaweza kula mara moja na kuwa umeshiba milele.
Unasafisha mwili wako kila siku.
Hakuna namna ya kuusafisha mara moja na ukawa msafi milele.
Ukitaka kupungua uzito unafanya mazoezi kila siku.
Ukitaka kupata utajiri unaongeza kipato na kuweka akiba kila siku.
Kila kitu kwenye maisha ni matokeo ya tabia endelevu ambavyo imefanywa kwa muda mrefu.
Hivyo chochote unachotaka kujenga, jikumbushe kitachukua muda kutengamaa.
Achana kabisa na kutafuta njia za mkato za kupata chochote unachotaka.
Kila kitu chenye maana kinahitaji juhudi na muda mpaka kukamilika.
Hatua ya kuchukua;
Angalia ni tabia zipi unazohitaji kujijengea ili kuweza kupata matokeo makubwa unayoyataka.
Jenga tabia hizo ukijua zitaleta matokeo makubwa.
Tafakari;
Hakuna kitu chochote kizuri na cha thamani ambacho kimewahi kuwa rahisi.
Ni lazima mtu ujitoe sana ndiyo uweze kupata kile chenye manufaa.
Je wewe umejitoa kiasi gani?
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed