#SheriaYaLeo (242/366); Waambukize hisia sahihi.
Sisi binadamu ni viumbe wa kihisia ambapo maamuzi yetu huwa tunayafanya kwa kusukumwa na hisia.
Kama unataka kuwashawishi watu, itakuwa rahisi kwako kama utaanza kwa kugusa hisia zao.
Na njia rahisi ya kugusa hisia ni kwa kuziambukiza.
Anza kwa kuwa na zile hisia ambazo unataka watu wawe nazo ili waweze kufanya maamuzi kwenye kile unachowashawishi.
Kwa kuwa hisia huwa zinaambukizwa, kwa kuanza na hisia hizo, watu wanaziiga kutoka kwako na wanakuwa rahisi kushawishika.
Moja ya hisia unazoweza kutumia ni kuwakubali watu kama walivyo na kuonyesha kuwajali kweli.
Kwa kufanya hivyo watu hao nao wanasukumwa kukukubali na kukujali kweli.
Ni katika hali hiyo ya kukukubali na kukujali ndiyo watu wanakuwa rahisi kushawishika na wewe.
Sheria ya leo; Kama viumbe wa kihisia na kijamii, huwa tunaathiriwa sana na hisia za watu wengine. Tumia nguvu hii kuwaambukiza watu hisia ambazo zitawafanya wawe rahisi kushawishika na wewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji