2742; Hawaoni unachoona.

Kuna mahali unayaona maisha yako yakiwa yamefika.
Hakuna mwingine yeyote mwenye maono ya aina hiyo.

Watu wengine wanapokushauri, hawakushauri kulingana n maono makubwa uliyonayo ndani yako.
Bali wanakushauri kwa vile wanavyoona itakupendeza zaidi.

Lakini siyo kinachokupendeza ndiyo chenye manufaa kwako.
Bali kile kinachoendana na maono makubwa uliyonayo kwenye maisha yako.

Kwa kujua hilo, ni muhimu sana kuhoji kila aina ya ushauri unaopokea kutoka kwa wengine kabla hujauchukua na kuufanyia kazi.
Nini msukumo wao, kukufurahisha au kukukuza zaidi?
Ni mara chachee sana vyote vinaweza kuwa pamoja.
Mara nyingi uwepo wa kimoja unakuwa umekiondoa kingine.

Unachotaka wewe ni kuyafikia maono makubwa uliyonayo.
Hivyo tengeneza udhibitii ambao utakuwezesha kukamilisha hilo bila ya kukwama popote pale.

Pia kuwa makini na ushauri unaopewa na wengine.
Wanaweza kuwa na nia nzuri na bado ushauri wao ukawa na madhara makubwa kwako.

Hatua ya kuchukua;
Kwa kila maamuzi unayofanya kwenye maisha yako, hakikisha unahusisha maono yako makubwa uliyonayo.
Hayo ndiyo yanapaswa kuwa chujio kwenye kila unachokutana nacho.

Tafakari;
Bila ya maono watu hupotea.
Kwa sababu wanakosa msingi wa kusimamia na kuutumia kufanya maamuzi yoyote ya maisha yako.
Kila mtu anakutana na mengi kwenye maisha yake.
Bila ya kuwa na chujio sahihi utazolewa na kila aina ya mafuriko yanayoendelea kwenye maisha.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed