#SheriaYaLeo (246/366); Dhibiti mchezo mzima.
Maisha ni kama mchezo wa drafti.
Anayefanikiwa ni yule anayekuwa na udhibiti kwenye mchezo mzima.
Kila kete inachezwa kwa kusudi maalumu, ambalo ni kupata ushindi mkubwa baadaye.
Hivyo ndivyo maisha yanavyokuwa.
Hakun hatua yoyote inayochukuliwa kwa kubahatisha.
Badala yake kila hatua inakuwa imepimwa na kupangiliwa kwa namna ambayo udhibiti unakuwa mkubwa na matokeo mazuri.
Hupaswi kuruhusu wengine kuvuruga mipango na mikakati uliyonayo.
Na pia hupaswi kuonekana wazi wazi unawalazimisha watu kwa namna fulani.
Hapo ndipo unapokuwa unahitajika kuwa na mkakati unaokupa wewe udhibiti mkubwa kwenye kile unachofanya na kila hatua unayochukua inawasukuma wengine kwa namna fulani bora zaidi.
Jenga udhibiti mkubwa kwenye kila anachofanya, ukiyajua matokeo unayotaka kufikia na kutoruhusu mtu yeyote kuingilia hilo.
Sheria ya leo; Kuwa na udhibiti mkubwa kwenye hisia zako mwenyewe na weka mikakati yako mapema na usiruhusu yeyote kuiharibu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji