2743; Kuuza ni wajibu wako.
Pata picha, una tiba ya ugonjwa fulani ambao unawasumbua sana watu.
Tiba hiyo ni ya uhakika kabisa, lakini watu bado hawajui na wengi badk hawaiamini.
Katika hali kama hiyo, kuuza dawa yako unakuwa ni wajibu mkubwa kwako.
Kwa kila anayeteseka na ugonjwa huo ila hajapata tiba uliyo nayo anakuwa ni wajibu kwako kuhakikisha ameipata.
Na hata pale unapomweleza mteja matibabu uliyonayo ila akakataa, bado ni wajibu wako kuhakikisha ameelewa na kupata tiba hiyo kwa kuwa unajua ina manufaa kwake.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa chochote unachouza.
Kina umuhimu mkubwa kwa wale unaowauzia.
Hata kama hawajakijua au wanakuw wabishi unapowaelezea, jua ni wajibu wako kuhakikisha watu hao wanakipata kitu hicho.
Kama muuzaji, unapaswa kujua huuzi tu kwa sababu unataka fedha.
Bali unauza kwa sababu kile ulichonacho kina manufaa makubwa kwa wale unaowalenga.
Ona ni wajibu wako kabisa kuhakikisha wale unaowalenga wanapata kile unachouza ili uwajibike katika kuwapatia kitu hicho.
Hatua ya kuchukua;
Kwa kile unachouza, acha kukiangalia kama njia ya wewe kupata fedha, bali kiangalie kama sehemu ya wewe kuwa na mchango bora kabisa kwa ajili ya wengine. Ona ni jinsi gani unayafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi kupitia kile unachouza. Kisha kiuze kwa kujivunia kwani ni mchango wako bora kwa wengine.
Tafakari;
Kuuza siyo tu njia ya mtu kupata fedha anazokuwa anazihitaji sana. Bali pia kuuza ni sshemu ya kutoa mchango mzuri kwa wengine, kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi.
Je, kile unachouza wewe kina manufaa gani makubwa kwa wale unaowalenga?
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed