#SheriaYaLeo (247/366); Piga kwenye mhimili.

Ni kawaida ya mamlaka kuonyesha uimara wake kwa lengo la kutisha au kuhadaa wengine.
Hakuna mamlaka inayopenda kuonyesha udhaifu wake, japo kila mamlaka ina udhaifu.

Kila mamlaka huwa ina mhimili wake, ambapo ndiyo uimara na nguvu za mamlaka hiyo vimejikusanya.
Huo ndiyo mhimili ambao unakuwa umeshikilia mamlaka hiyo.

Kushambulia mhimili mkuu wa mamlaka ndiyo mkamati wa uhakika wa kupata ushindi.
Mhimili huo unapotikisika mamlaka inapata udhaifu na kuwa rahisi kuanguka.

Kupiga kwenye mhimili wa mamlaka ndiyo njia bora ya kumaliza mgogoro kwa uhakika.

Lakini kila mamlaka huwa inaficha mhimili wake, kwa sababu hapo ndipo penye nguvu na udhaifu pia.
Ili kujua ulipo mhimili, kuwa makini usipotoshwe na maonyesho ya nje ambayo kila mamlaka huwa inayafanya.

Utapaswa kuchukua hatua moja baada ya nyingine ili kuweza kujua ulipo mhimili mkuu na kupiga hapo ndiyo uweze kupata ushindi.

Sheria ya leo; Unapowaangalia wapinzani wako, tafuta ulipo mhimili unaoshikilia mamlaka yao yote. Mhimili huo unaweza kuwa utajiri wao, umaarufu wao, nafasi waliyonayo au mkakati wao wa ushindi. Kuwapiga kwenye huo mhimili kunaangusha mamlaka kwa urahisi zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji