2746; Kutamani, kupanga na kufanya.

Matamanio ni bure kabisa, kila mtu huwa anatamani kuwa na vitu vizuri.
Ni matamanio ya kila binadamu kupata mafanikio makubwa.

Kupanga ni rahisi, watu wengi huwa wanaweka mipango mizuri kabisa ya kupata kile wanachotamani.
Wanakuwa wanajua nini wanapaswa kufanya ili kupata wanachotaka.

Tatizo kubwa lipo kwenye kufanya, ni wachache sana wanaofanya, wanaochukua hatua kwenye matamanio na mipango yao.

Na katika hao wachache wanaofanya, ni wachache zaidi ambao wanafanya kwa msimamo.
Yaani wanapanga na kufanya kama walivyopanga bila ya kutetereka.

Haishangazi kwa nini wanaoishia kufanikiwa ni wachache mno kati ya wengi ambao wanayatamani mafanikio na hata kwenda mbali na kupanga kuyapata.

Kinacholeta matokeo siyo kutamani wala kupanga, bali kufanya.
Na siyo tu kufanya, bali kufanya kwa msimamo.
Kama kuna kitu unataka kwenye maisha yako na hujakipata, tatizo ni hujafanya ili kukipata kitu hicho.

Hatua ya kuchukua;
Jiulize ni nini hasa unachotaka kupata au kufikia kwenye maisha yako.
Kisha jiulize nini unapaswa kufanya ili kupata unachotaka.
Na kinachofuata baada ya hapo ni kufanya kama ulivyopanga mara zote bila kuacha.
Fanya bila kuacha.
Fanya kwa ubora zaidi mara zote.
Ni kwa kufanya ndiyo unaweza kupata chochote unachotaka.

Tafakari;
Kama matokeo unayoyapata ni tofauti na unayoyataka, basi jua hujafanya kile unachopaswa kwa msimamo wa kutosha.
Angalia ni wapi ambapo hufanyi, kisha fanya kwa msimamo mkubwa.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed