#SheriaYaLeo (250/366); Usimshambulie adui kwenye uimara wake.
Kile ambacho adui anakionyesha wazi wazi ndiyo uimara wake.
Ukimshambulia kwenye hicho huwezi kumshinda, bali utamfanya azidi kuwa imara.
Njia pekee ya kumshinda adui yeyote yule ni kumshambulia kwenye madhaifu yake.
Kila mtu ana madhaifu, ambayo huwa anajaribu kuyaficha.
Hivyo chochote anachokionyesha mtu jua ndiyo uimara wake na ambao unaficha madhaifu yake.
Ni kwa kuyajua madhaifu yake na kuyatumia ndiyo unaweza kumshinda adui.
Wajibu wako mkubwa ni kuyajua madhaifu waliyonayo maadui zako na kuyashambulia hayo.
Kwa kufanya hivyo unawavuruga, unawaondoa kwenye utulivu wao wa kukushambulia na kuwafanya wakazane kujilinda.
Kamwe usimkabili adui au mshindani kwa kile anachokuonyesha, bali nenda kwenye kile anachoficha.
Ni kwenye kile anachoficha ndipo udhaifu mkubwa upo na unapoweza kupata ushindi.
Sheria ya leo; Unapowakabili watu kwenye uimara wao, unawafanya wazidi kuwa na upinzani mkali na hivyo kuwa vigumu kwako kushinda. Unachopaswa kufanya ni kuwakabili kwenye madhaifu yao, hapo unawavuruga, unapunguza upinzani na kufanya ushindi kuwa rahisi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji