#SheriaYaLeo (259/366); Achana na mazoea.
Majenerali bora wa kivita na wanamikakati wabunifu huwa wanafanikiwa siyo kwa sababu ya ujuzi walionao, ila kwa sababu wanaweza kuachana na mazoea na kuweka umakini wao kwenye wakati uliopo.
Hivyo ndivyo ubunifu unavyochochewa na fursa kutumiwa.
Maarifa, ujuzi na uzoefu huwa vina ukomo. Hakuna kiwango cha kufikiri kinachoweza kukuandaa na changamoto mbalimbali za maisha.
Mara zote mipango yetu huwa inatofautiana na uhalisia.
Haijalishi tumepanga na kujiandaa kwa namna gani, uhalisia huwa unakuwa tofauti kabisa na mipango yetu.
Hivyo ili ufanikiwe lazima uwe tayari kubadilika kulingana na uhalisia unaokutana nao badala tu ya kubaki kwenye mipango ya awali na mazoea.
Kuendelea kung’ang’ana na mipango ya awali wakati uhalisia upo tofauti ni kuchagua kushindwa.
Badala ya kutumia muda mwingi kuchambua makosa ya nyuma ni bora kujenga uwezo wa kufikiri kulingana na uhalisia na kuchukua hatua sahihi badala ya kwenda na mazoea.
Kwa njia hiyo utapunguza makosa ya kuchambua.
Sheria ya leo; Chukulia akili kama mto; kadiri unavyotiririka kwa kasi, ndivyo unavyokabiliana na mambo yaliyopo pamoja na mabadiliko. Achana na mazoea na endana na uhalisia ili kufanya maamuzi sahihi kila wakati.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji