#SheriaYaLeo (263/366); Tumia wengine kukamilisha yasiyo mazuri.
Kama kuna mambo ambayo siyo mazuri yanapaswa kufanyika, hupaswi kuyafanya wewe mwenyewe, kwa sababu yataharibu sifa yako na kuwa kikwazo kwako.
Badala yake unapaswa kuwatumia watu wengine kukamilisha mambo hayo.
Kwa namna hiyo lawama zitaenda kwa watu hao wengine, huku wewe ukibaki na sifa nzuri.
Tujifunze kutoka kwenye hekaya, ambapo nyani alikuwa anataka kupata karanga kutoka kwenye moto lakini hakuwa tayari kuungua.
Alichofanya ni kutumia mguu wa paka kutoa karanga hizo kwenye moto.
Hivyo nyani akaweza kupata karanga alizotaka bila ya kuungua yeye mwenyewe.
Usijiweke kwenye hatari kwa kufanya vitu ambavyo vinaweza kuharibu sifa yako.
Badala yake watumie watu wengine kukamilisha mambo ya aina hiyo.
Watu wa aina hiyo wanakusaidia kukamilisha yale muhimu bila ya watu kujua kama wewe ndiye unayehusika.
Sheria ya leo; Wacha wengine wawe ndiyo wakamilishaji wa mambo yasiyo mazuri au watoaji wa taarifa zisizo nzuri. Wakati wewe unaonekana kukamilisha mazuri na kuleta taarifa nzuri.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji