#SheriaYaLeo (264/366); Fanya tofauti na ulivyozoea.
Watu huwa wanategemea tabia zako zifanane na za watu wengine.
Wajibu wako kama mwanamkakati bora ni kwenda kinyume na mazoea hayo.
Washangaze watu kwa kufanya tofauti na vile ilivyozoelela.
Kwa Sun Tzu na wanamikakati wengine, kufanya kitu cha tofauti bila ya utangulizi wa kitu cha kawaida ni kuchagua kushindwa.
Lazima kwanza utangulize kilichozoeleka ili kuwaandaa watu kisha kwenda kwenye kile ambacho hakijazoeleka ili kuwa na ushawishi zaidi.
Kwa kuanza na mazoea, inakuwa rahisi zaidi kuwashawishi watu pale unapofanya kinyume na mazoea.
Sheria ya leo; Fanya mambo yako kwa mipango yako mwenyewe. Usifuate mazoea ya wengine, badala yake fanya kwa utofauti na hilo litafanya iwe vigumu kwa watu kuweza kutabiri nini utafanya.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji