2772; Uzuri wa ukweli.
Uzuri wa kusema ukweli ni kwamba huhitaji kuweka kumbukumbu yoyote ile kwenye yale unayoongea.
Kwa sababu ukweli hubaki hivyo daima, huhitaji kujiuliza mara mbili mbili kabla ya kusema kitu.
Unaposema uongo inabidi uwe na kumbukumbu nzuri ili kukumbuka yote ambayo umeshayadanganya kuepuka kusema kitu cha tofauti.
Sasa kwa kuwa kumbukumbu zetu sisi binadamu siyo bora, huwa tunaishia kusema vitu ambavyo vinaweka hadharani uongo ambao tumekuwa tunausema.
Kwa kuangalia jinsi njia ya uongo ilivyo fupi, tunazidi kuona jinsi ukweli unavyo na umuhimu.
Hivyo tunakuwa upande samala zaidi kama tutasimamia ukweli mara zote.
Kusimamia ukweli mara zote siyo zoezi rahisi.
Mara nyingi ukweli unaumiza manzoni na kumnyima mtu kile anachotaka.
Lakini mbeleni ukweli huo unakuweka huru na kukupa matokeo mazuri kuliko ungetumia uongo.
Kusimama kwenye ukweli mara zote ni hitaji muhimu sana kwenye hii safari ya mafanikio.
Kila unaposimama kwenye ukweli unaimarisha zaidi matokeo yako ya mbele.
Hatua ya kuchukua;
Jiulize umekuwa unasimama kwenye ukweli kwa kiasi gani?
Msimamo kwenye ukweli ni kitu ambacho kitakupa manufaa makubwa zaidi.
Mara zote simama kwenye ukweli.
Tafakari;
Kwa kusema ukweli, unaweza kuona kama kuna vitu unapoteza, lakini hilo ni kwa muda mfupi tu, baadaye matokeo yanakuwa mazuri.
Kwa kusema uongo unaweza kuona kama kuna manufaa unayapata, lakini hayo ni kwa muda mfupi tu, baadaye maumivu na hasara vinakuwa kwa kiwango kikubwa.
Simama kwenye ukweli mara zote, unakipa.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed