#SheriaYaLeo (284/366); Fikiri kwa ajili yako mwenyewe.

Sisi binadamu huwa tunapenda sana vitu ambavyo ni rahisi na tumeshavizoea.
Tunayapata mawazo yetu kutoka kwa wazazi, shule na jamii inayotuzunguka.
Na mitandao ya kijamii imezidisha sana hali hiyo ya kutegemea fikra za wengine.

Hivyo ndivyo tunavyoishia kufikiri kuhusu dunia na maisha kwa ujumla.
Tunaacha kufikiri sisi wenyewe na kuiga kile wengine wanachofanya na kufikiri.
Tunaishia kuwa waoga wa kufikiri kwa akili zetu wenyewe.

Hivyo ndivyo watu wengi wanayaendesha maisha yao.
Kufuata kile kilichozoeleka badala ya kufikiri na kuja na ambacho ni kipya na tofauti.

Unapaswa kuondokana na hofu hizo zinazokuweka kwenye ukawaida na kuanza kufikiri kwa akili yako na kuja na mawazo ambayo ni ya tofauti kabisa.
Lazima uwe tayari kuachana na mazoea yote ambayo yamekuwa yanarahisisha maisha yako.

Fikiri kwa akili yako na ajili yako mwenyewe.
Hivyo ndivyo utakavyoweza kupata matokeo bora na ya tofauti.

Sheria ya leo; Unapaswa kufikiri kwa ajili yako mwenyewe na kutokukubali kufungwa na fikra za wengine. Hiyo ndiyo njia ya uhakika ya kujitofautisha na wengine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji