#SheriaYaLeo (287/366); Kubadili matokeo badili mtazamo wako.

Jinsi ambavyo unaona na kuchukulia vitu, siyo jinsi ambavyo vilivyo, bali ni jinsi wewe mwenyewe ulivyo, mtazamo ambao unao.

Hiyo ndiyo maana unaweza kuwakuta watu wawili wako kwenye eneo moja, wakifanya kitu kinachofanana, mmoja akawa amefanikiwa na mwenye furaha huku mwingine akiwa ameshindwa na asiye na furaha.

Jinsi unavyoiona dunia kwa nje inatokana na vile unavyojiona wewe mwenyewe kwa ndani.
Hivyo kama unataka kubadili matokeo unayopata, unapaswa kufuata mchakato sihihi kwako ambao unaanza kwa kubadili mtazamo wako kwanza.

Dunia ipo kama ilivyo, vitu siyo vizuri wala vibaya, siyo vigumu wala rahisi.
Mtazamo ambao mtu unakuwa nao ndiyo unakuwa kama miwani yenye rangi unayoweza kudhani ndiyo ukweli.

Kwa kuwa unaona tu kile unachotaka kuona, unapaswa kuweka juhudi kubwa kujijengea mtazamo sahihi.
Jijengee mtazamo chanya na utumie kwenye kila jambo ili uweze kupata msukumo mkubwa wa kuyanya yale yaliyo sahihi.

Sheria ya leo; Tuna nguvu kubwa ya kuweza kubadili matokeo tunayopata na namna wengine wanavyotuchukukia kama tutabadili mtazamo tulionao. Huoni vitu jinsi vilivyo, bali jinsi wewe ulivyo . Anza kwa kubadilika wewe na vinavyokuzunguka vitabadikika.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji