Rafiki yangu mpendwa,

Waswahili wanasema usiandikie mate wakati wino upo.

Hii ni kauli inayotutaka tuthibitishe mambo sisi wenyewe badala tu ya kudhani au kuenda na mazoea.

Inapokuja kwenye fedha, kuna kauli moja maarufu ambayo imekuwa ikitolewa sana.

Kauli hiyo ni fedha haiwezi kununua furaha.

Sasa hapa sitaki kujadili kama kauli hiyo ni kweli au si kweli.

Ila ninachotaka kukuambia ni badala ya kuichukua na kuiamini ilivyo, ithibitishe mwenyewe.

Labda ni kweli fedha hainunui furaha, lakini kwa nini kwanza usiipate ya kutosha ukajithibitishia mwenyewe?

Kwa sababu kupata fedha siyo kilema kwamba ukishakipata ndiyo utabaki nacho maisha yako yote.

Nakupa huu mpango,
Jipe miaka 10 ya kupambana kufika kwenye uhuru wa kifedha.
Weka juhudi kubwa kwenye njia uliyochagua kujenga utajiri wako.
Usichukue ushauri wowote wa kukukatisha tamaa kwenye hilo.

Kisha baada ya kupata utajiri huo na uhuru wa kifedha, pima wewe mwenyewe.
Je umekuletea furaha? Kama jibu ni ndiyo endelea nao.
Na kama jibu ni siyo basi toa utajiri wako wote kama msaada kwa wenye uhitaji.

Huo ni mpango wenye manufaa.
Maana ukipata utajiri na ukaufurahia inakuwa bora kwako.
Na kama utapata utajiri na usiufurahie, utakapotoa msaada utakuwa umewanufaisha wengine.

Je umekubali mpango huo?
Kama ndiyo basi makushauri uwe na vitabu vitatu vya mwongozo;
1. ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.
2. ELIMJ YA MSINGI YA BIASHARA.
3. MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.

Jibu ujumbe huu kwa kuandika namba yako ya simu na nitakupa mpango mzuri wa kuvipata vitabu hivyo.
Au tuwasiliane; 0752 977 170.

Kocha.