#SheriaYaLeo (293/366); Wakubali watu kama walivyo.

Kuchangamana na watu wengine ndiyo moja ya chanzo kikuu cha matatizo ya kihisia, lakini haipaswi kuwa hivyo.

Tatizo ni kwamba huwa tunawahukumu watu mara zote, tukitamani wangekuwa tofauti na walivyo.

Huwa tunataka kuwabadili watu, tukitaka wafikiri na kufanya kama sisi.
Lakini hilo huwa haliwezekani, kwa sababu huwa tunatofautiana.
Hilo ndiyo huwa linatuvuruga sana.

Njia bora ya kukabiliana na hilo ni kuacha kuwahukumu watu na kuwapokea vile walivyo.
Kuacha kuwachukukia chanya au hasi, badala yake kuwachukulia kwa namna walivyo, kama unavyochukulia jiwe au mti.

Badala ya kulalamika watu wako tofauti, tumia kile walichonacho.
Kutofautiana kwa watu ndiyo kunayafanya maisha yawe bora na ya kusisimua.

Chukulia kuwaelewa watu kama mchezo wa kuielewa asili ya binadamu na kuweza kuitumia vyema.
Ndiyo watu wanaendeshwa na hisia badala ya mantiki, lakini hivyo ndivyo na wewe ulivyo pia.

Madhaifu unayoyaona kwa wengine, jua yapo na kwako pia.
Kutambua hilo na kuwakubali watu jinsi walivyo badala ya kujaribu kuwabadilisha, itakupa uhuru na utulivu mkubwa.

Sheria ya leo; Chunguza makosa unayoyaona kwa wengine na uone jinsi yalivyo na kwako pia. Kwa kujua hilo, unapaswa kuwakubali watu kama walivyo, badala ya kutamani wangekuwa tofauti au kutaka kuwabadilisha wawe vile unavyotaka wewe.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji