2796; Uhakika kwamba unaweza kufanikiwa.
Thomas Edison amewahi kunukuliwa akisema; “Kama tungefanya mambo yote tunayoweza kufanya, tungejishangaza wenyewe.”
Sina cha kuongeza hapo, tunaenda moja kwa moja kwenye hatua ya kuchukua.
Hatua ya kuchukua;
Chukua kalamu na karatasi na orodhesha mambo yote unayoweza kufanya kwenye biashara au kazi yako.
Orodhesha yote bila kuacha hata moja.
Anza kufanyia kazi orodha hiyo kwa msimamo bila kuacha.
Anza na vichache na nenda ukiongeza mpaka ukamilishe yote.
Halafu niambie kama hutajishangaza.
Tafakari;
Popote ulipofika sasa, ni matokeo ya yale uliyofanya au kutokufanya huko nyuma. Kujua tayari unajua, kuweza tayari unaweza, ni kufanya ndipo unakwama.
Jijengee nidhamu na msimamo wa kufanya na utaona jinsi mabadiliko makubwa yatakavyokuja kwako.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed