2798; Mazoezi na vita.

Kabla ya wanajeshi kwenda vitani huwa wanafanya mazoezi makali.
Mazoezi ambayo yanajaribu kuiga uhalisia wa yale watakayokutana nayo kwenye vita.

Kabla wachezaji hawajaingia kwenye mashindano, huwa wanafanya mazoezi makali. Mazoezi hayo hugusa kila hali ambayo watakutana nayo kwenye mashindano.

Mazoezi yana nguvu ya kumjengea mtu uzoefu wa kukabiliana na hali anazokutana nazo.

Bila mazoezi unaweza kudhani unajua kitu, lakini ni mpaka unapohitajika kukifanyia kazi ndiyo unajua kiasi gani umekuwa hujui.

Maisha ni vita, maisha ni mchezo. Swali ni una mazoezi kiasi gani kabla hujaendelea na maisha hayo?

Kwa sababu kinachopelekea changamoto nyingi tunazokutana nazo kwenye maisha zituzidi ni kukosa mazoezi.

Tunajifariji tayari tunajua, ila kujua bila kufanya mazoezi, hakuna unachojua. Na hilo litajidhihirisha wazi pale unapokutana na hali inayokutaka uyatumie hayo unayojiambia unayajua.

Hatua ya kuchukua;
Weka juhudi nyingi kwenye mazoezi ili uweze kukabiliana na hali yoyote unayoweza kukutana nayo.
Usikubali kuwa ndiyo unakutana na chochote kwa mara ya kwanza, kitakuwa na nguvu ya kukusumbua.

Tafakari;
Kanuni ya ugumu na urahisi inaendelea kutumika. Mazoezi yakiwa rahisi, vita inakuwa ngumu. Na mazoezi yakiwa magumu, vita inakuwa rahisi.
Ni wewe tu uchague unataka ugumu wapi na urahisi wapi.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed