#SheriaYaLeo (302/366);Sogelea unachokionea wivu.
Watu huwa wana tabia ya kuficha matatizo yao na kuonyesha nyuso zenye furaha.
Tunachoona na kusikia kwa watu ni habari njema na ushindi.
Hilo huwa linajenga hali ya wivu kwetu, kwa kuona wengine wapo pazuri kuliko pale tulipo sisi.
Lakini kama tutawasogelea karibu hao tunaowaonea wivu, kama tutawajua kwa undani zaidi, tutagundua mambo yaliyo ndani ni tofauti na yale yanayoonyeshwa nje.
Kwa kuona uhalisia huo wa ndani kutafanya usiendelee kuwa na wivu juu ya watu au vitu.
Kwa yale unayokuwa umeyaona kwa kuchunguza ndani, hutatamani na wewe kuyapitia.
Vitu vingi ambavyo watu wanaonyesha kwa nje huwa ni tofauti na uhalisia wa ndani.
Hakuna kitu chenye ukamilifu kama unaoonekana kwa nje.
Kama unakionea kitu wivu kwa yale unayoona nje, jua unajidanganya.
Taka kujua kwanza ndani na utajionea mwenyewe huna sababu ya kuwa na wivu, maana hutayataka yale uliyoyaona.
Sheria ya leo; Kumbuka kwamba ni watu wachache sana ambao kweli wana furaha kama wanavyoonyesha kwa nje, wengi sana wanachoonyesha kwa nje ni tofauti na ndani. Ona kwa undani kabla hujawa na wivu kwenye chochote kile.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji