#SheriaYaLeo (304/366); Asili ya binadamu haibadiliki.
Dunia inaendelea kupiga hatua.
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaleta ufahamu kwenye mambo mengi ambayo huko nyuma hayakujulikana.
Kwa sababu hiyo tunaweza kudhani pia kwamba binadamu nao wanabadilika.
Lakini ukweli ni kwamba asili ya binadamu huwa haibadiliki.
Bado watu wanafanya maamuzi kwa hisia badala ya mantiki.
Bado watu wanafuata mkumbo badala ya kusimamia kile kilicho sahihi.
Na bado watu wanaamini kwenye mambo ambayo kisayansi yameshathibitishwa kwamba siyo sahihi.
Kwa kuwa asili ya binadamu ni ngumu kubadilika, hasa inapokuja kwenye kundi, ni vyema mtu kujitathmini kila mara ili usikwamishwe na asili hiyo.
Na hatua ya kwanza na muhimu ya kuhakikisha hukwamishwi na asili yetu binadamu ni kuepuka kufanya maamuzi kwa kuiga au kufuata mkumbo.
Mara nyingi sana kitu kinachokubalika na wengi huwa siyo kilicho sahihi.
Sheria ya leo; Asili ya binadamu haibadiliki, ukitaka asili hiyo isiwe kikwazo kwako, epuka kufanya maamuzi kwa mkumbo. Mara zote jitathminj kwa namna unavyofanya mambo yako ili kuhakikisha hukwamishwi na asili yetu binadamu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji