#SheriaYaLeo (305/366); Wewe ndiyo kikwazo kwako.
Maisha ni vita na mapambano, kila wakati unajikuta ukikabiliana na hali mbaya, mahusiano mabovu na mashirikiano hatari.
Jinsi unavyokabiliana na hali hizo ndiyo itaamua hatima yako.
Kama utajiona umepotea, kama utapoteza mwelekeo, kama huwezi kutofautisha rafiki na adui, unapaswa kujilaumu mwenyewe.
Kila kitu kwenye maisha kinategemea mtazamo wako wa kiakili na jinsi unavyoiangalia dunia.
Kubadili mtazamo kuna kugeuza kutoka kuwa mamluki na kwenda kuwa mpambanaji mahiri.
Kama kuna jambo lolote ambalo unakwama kwenye maisha yako, wewe mwenyewe ndiye kikwazo kwako.
Mtazamo unaokuwa nao ndiyo kinakuwa kikwazo kikubwa kwako.
Kwa kuanza na kubadili mtazamo wako, utaweza kuvuka vikwazo vingi kwenye maisha yako.
Sheria ya leo; Kikwazo kikubwa kwako siyo mito, milima au watu wengine; kikwazo kikuu kwako ni wewe mwenyewe. Kwa kuanza na wewe mwenyewe, utaweza kuvuka mengi ambayo yamekuwa yanakuzuia usipate unachotaka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji