2810; Usitengeneze majuto.
Unakumbuka ukiwa shuleni, kuna wakati ulikuwa husomi sana na pale matokeo yalipokuwa yanatoka ukawa unajiambia kama ungeweka juhudi zaidi, ungeweza kupata matokeo zaidi?
Hiyo ni dhana ambayo wengi wanaondoka nayo shuleni na kwenda nayo kwenye maisha, kitu kinachowazuia wasipate mafanikio makubwa.
Kufanya vitu nusu nusu ili ukishindwa uwe na kisingizio kwamba kama ungeweka juhudi kamili ungepata matokeo bora zaidi!
Hilo halikusaidii chochote zaidi ya kukutengenezea majuto kwenye maisha.
Na majuto hayo hayawezi kukupa mafanikio unayotaka, zaidi tu yatakupa maumivu.
Kwenye safari yako ya mafanikio, hakikisha hutengenezi majuto ya aina yoyote.
Wewe fanya kila unachopaswa kufanya, tena kwa viwango vya juu kabisa.
Na hata kama matokeo yatakuja tofauti na ulivyotegemea, ndani yako unakuwa huna majuto, unajua ulifanya kila ulichopaswa kufanya.
Kufanya kila unachopaswa kufanya haitakuhakikishia matokeo unayotaka. Lakini itakuweka kwenye nafasi nzuri ya kupata fursa bora zaidi za kupata unachotaka.
Lakini ukienda kwa kujitegea, kujua unachopaswa kufanya lakini hufanyi, unaishia kupata matokeo ya chini na kushindwa.
Kwa kila unachochagua kufanya, weka kila unachopaswa kuweka.
Usijizuie wala kujipunguzia hata kidogo.
Fanya kila kitu kiasi kwamba hata matokeo yaje kwa namna gani, hutakuwa na majuto.
Hatua ya kuchukua;
Leo jiulize ni vitu gani ambavyo unajua kabisa unapaswa kuvifanya, lakini umekuwa huvifanyi kwa ukamilifu wake?
Hapo ndipo unapotengeneza majuto na kujizuia kufanikiwa.
Amua leo unakwenda kufanya yote unayopaswa kufanya kwenye kile ulichochagua na huachi nafasi ya kutengeneza majuto.
Kwa kuwa hakuna juhudi unazoweka zikapotea, kujitoa kwako kutaleta matokeo bora zaidi.
Tafakari;
Wahenga walisema majuto ni mjukuu. Hutayaona wakati unafanya jambo, bali yanakuja kutokea baadaye ukiwa huna tena namna ya kuathiri jambo hilo. Sasa wewe usikubali kujenga majuto ya baadaye, hivyo hakikisha unafanya kila unachopaswa kufanya na kwa viwango vya juu kabisa.
Na hata kama matokeo yatakuja tofauti, unajua ulifanya kila ulichopaswa. Na kila wakati utaendelea kufanya hivyo.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed
Asante Kocha.
LikeLike