#SheriaYaLeo (317/366); Vunja agano la mazoea.

Kuna mazoea ambayo tayari yameshajengeka na yanazingatiwa sana kwenye jamii.
Jinsi watu wanavyopaswa kuwa, vitu wanavyopaswa kusema na kufanya tayari vimeainishwa.
Hali hizo zinakuwa zimejengwa kwenye tofauti za kijinsia, kikabila, kielimu na nyinginezo.

Kukaa kwenye maagano haya ya mazoea ni kujizuia usifanye makubwa, kwani unakuwa umejiwekea ukomo wewe mwenyewe.
Unaweza kuwa unataka kusema au kufanya kitu fulani, lakini mazoea yaliyowekwa yakawa yanakuzuia.
Labda ni kutokana na jinsia, umri au kiwango cha elimu.

Unapaswa kuvunja maagano hayo ya mazoea ili uwe huru kufanya kile unachotaka kufanya.
Unapaswa kuwa wewe halisi, kufanya kile chenye msukumo mkubwa ndani yako.
Hicho ndiyo kitakutofautisha na wengine na kukupa matokeo ya tofauti.

Usikubali mazoea yaliyowekwa kwenye jamii kuwa kikwazo kwako kuyaishi maisha yako.
Kuwa wewe, hiyo ndiyo njia pekee ya kufanya makubwa.

Sheria ya leo; Onyesha kivuli chako. Fungua nguvu kubwa na ya kipekee iliyo ndani yako na usikubali kuzuiwa na mazoea ya kijamii.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji