#SheriaYaLeo (320/366); Kuwa na roho ya ukarimu.

Wote tumebeba majeraha na maumivu mbalimbali tangu utotoni.
Kwenye maisha yetu ya kijamii, kadiri tunavyokua, tunakutana na hali za kuangushwa na kukatishwa tamaa.
Hali hizo hutufanya tujione hatuna thamani na wala hatustahili vitu vizuri kwenye maisha.

Wote huwa tuna nyakati za wasiwasi juu yetu wenyewe. Nyakati hizo huwa zinatupa fikra na hisia kali za maumivu.
Hilo hutufanya tutafute njia ya kuzituliza fikra na hisia hizo na hapo ndipo wengi huzamia kwenye ulevi au tabia nyingine.
Lakini hilo limekuwa halisaidii, badala yale linatuweka kwenye gereza zaidi.

Ipo njia bora ya kuvuka hilo, njia ambayo inatuweka huru kutoka kwenye gereza hilo la fikra na hisia.
Njia hiyo inatokana na kubadili mtazamo na fikra zetu kuhusu dunia.
Hilo linaanzia kwenye kuwa na roho ga ukarimu, kwetu wenyewe na kwa wengine.
Kwa kuwakubali watu, kwa kuwaelewa na hata kuwapenda jinsi walivyo, tunazikomboa fikra na hisia zetu.

Tunaweza kuacha kulipuka kwa kila kitu ambacho watu wanasema na kufanya. Tunajipa nafasi na kuacha kuchukulia kila kitu binafsi.
Mabadiliko haya ya kimtazamo yanatupa uhuru mkubwa ambao unatuwezesha kufanya makubwa pia.

Sheria ya leo; Pale tunapokuwa wakarimu kwetu na kwa wengine, wanavutiwa kwetu na kutaka kuwa wakarimu pia.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji