2817; Uwajibikaji na Mchakato.
Unataka kufanikiwa?
1. Jua unachotaka.
2. Panga jinsi ya kukipata.
3. Chukua hatua.
4. Kaa kwenye mchakato.
5. Wajibika.
Unaanza kwa kujua nini unachotaka kwa uhakika kabisa.
Mafanikio kwako yana maana gani?
Hili lazima lianzie ndani yako, kwa kujisikiliza wewe mwenyewe.
Unaweza kushangaa, lakini ukweli ni sehemu kubwa ya watu hawajui nini wanachotaka kwa uhakika.
Ukishajua unachotaka, panga jinsi ya kukipata. Kwa kila unachotaka, kuna gharama unayopaswa kulipa. Wewe jua gharama ya kulipa kwenye mafanikio unayotaka, kisha amua kulipa gharama hiyo.
Ni lazima uwe na mpango unafikaje kwenye kile unachotaka.
Unapaswa kuchukua hatua kwenye mpango ulionao. Kujua unachotaka na kupanga ni asilimia 10 pekee ya safari.
Kuchukua hatua ndiyo asilimia 90 ya safari hiyo.
Unapaswa kufanya kile ulichopanga kufanya kama ulivyopanga.
Hupaswi kuwa mtu wa sababu na visingizio kwa nini umeshindwa kufanya.
Wewe fanya.
Kufanya mara moja pekee haitoshi kukupa mafanikio unayoyataka.
Unapaswa kufanya kwa kurudia rudia kwa muda mrefu bila kuacha au kukata tamaa.
Unapaswa kutengeneza mchakato wako kwenye ufanyaji na kisha kukaa kwenye mchakato huo kwa muda mrefu bila kuacha.
Kila juhudi unayoweka haipotei, bali inakuwa na mchango kwenye matokeo ya baadaye.
Uwajibikaji ni muhimu.
Pale unaposhindwa kufanya ulichopanga kufanya, unapaswa kuwajibika.
Uwajibikaji ndiyo unaokusukuma ufanye kama ulivyopanga bila kuruhusu sababu kuingilia.
Uwajibikaji utafanya ujisukume zaidi ya ulivyozoea.
Peke yako unaweza kushindwa kujiwajibisha vizuri.
Hivyo mara zote kuwa na mtu wa nje anayekuwajibisha.
Mchakato huu rahisi, ukikaa ndani yake kwa msimamo, hutabaki pale ulipo sasa.
Hatua ya kuchukua;
Andika mchakato wako wa kuyafikia mafanikio yako kwa mtiririko huu kisha tushirikishe kwenye maoni hapo chini.
Huo mchakato ulioandika ndiyo ramani yako, kaa humo.
Tafakari;
Bila ya mchakato, hakuna chochote kikubwa kinachowezekana kufanyika.
Amini kwenye mchakato, tengeneza mchakato wako na kaa kwenye mchakato huo. Hakuna kinachoweza kushinda mchakato unaofanyiwa kazi kwa uhakika.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed