#SheriaYaLeo (321/366); Tumia kivuli chako.
Tumeshaona jinsi ambavyo kila mtu ana kivuli ndani yako.
Sehemu ya nafsi ya mtu ambayo anapenda kuificha kwa sababu haikubaliki sana kwa wengine.
Nafsi hiyo huwa inakuwa na nguvu kubwa kama itaweza kutumiwa vizuri.
Hivyo wajibu wako ni kuangalia namna gani unavyoweza kutumia kivuli chako kufanya makubwa zaidi.
Usijione wa tofauti na kukata tamaa pale unapokuwa unaona kile ambacho wengine hawaoni.
Badala yake jumuisha nafsi zako zote na angalia jinsi unavyoweza kuzitumia kwa manufaa.
Vyovyote ulivyo unaweza kuwa na matumizi makubwa kwa wengine.
Acha kukandamiza nafsi hizo na badala yake zitumie kwa namna ambayo utakuwa na mchango bora zaidi kwa wengine.
Sheria ya leo; Lengo lako halipaswi tu kuwa kukubali na kupokea nafsi ya kivuli chako. Badala yake unapaswa kutumia kivuli hicho kufanya mambo ya tofauti na ya kipekee.
Kwa kufanya hivyo utakuwa umekamilika na kuwa wewe halisi ambaye hakuna wa kufanana na wewe. Na hapo ndipo unapoweza kufanya makubwa sana.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji