2820; Muda na fedha.
Kiashiria kizuri cha mtazamo wa kimafanikio wa mtu ni matumizi ya muda na fedha.
Wale wenye mtazamo wa kimasikini na wa kushindwa huwa wanatumia muda kuokoa fedha.
Hawa huona ni bora wapoteze muda kuliko fedha.
Dalili utakayoiona wazi ni jinsi watu hao wapo tayari kutumia muda mrefu kwenye kitu, kama tu kinawapa punguzo.
Mfano mzuri ni pale mtu anapoenda kununua kitu chenye punguzo la bei na kujikuta akipoteza muda mwingi kwenye hilo.
Wale wenye mtazamo wa kitajiri na wa kushinda huwa wanatumia fedha kuokoa muda.
Hawa kuona ni bora wapoteze fedha kuliko muda.
Watu hawa huepuka sana vitu vya bei rahisi, wakijua vitawahitaji kutumia muda mwingi kuvipata au kuvifanyia kazi.
Wanaamini unapata kile unacholipia na hivyo kuwa tayari kulipia bei juu ili kupata kilicho bora.
Hatua ya kuchukua;
Chunguza kila maamuzi unayofanya kuona msukumo wako ni upi, kuokoa muda au fedha?
Kuanzia sasa, angalia zaidi kuokoa muda kuliko fedha.
Upe muda wako thamani, kwa kuligawa lengo lako la fedha kwenye muda.
Kama lengo laki ni kipato cha milioni 5 kwa mwezi, hiyo ina maana kila siku ni laki moja na sabini. Kama unafanya kazi masaa 10 kwa siku, saa moja thamani yake inakuwa elfu 17.
Hiyo ina maana kwamba hupaswi kufanya chochote ambacho hakina thamani hiyo.
Tafakari;
Muda ni zaidi ya fedha, ni rasilimali yenye ukomo na uhaba mkubwa.
Ukipoteza fedha, unaweza kupata nyingine. Lakini ukipoteza muda, huwezi kuupata tena kamwe.
Usitumie muda kuokoa fedha, kufanya hivyo ni kutothamini muda wako na kujizuia usifanikiwe.
Tumia fedha kuokoa muda na muda huo ukiutumia vyema utaweza kufanya makubwa sana.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed