#SheriaYaLeo (324/366); Hatima ya maisha yako.
Watu wote waliowahi kufanya makubwa hapa duniani walikuwa ni watu wa kuamini maisha yao yana hatima kubwa.
Hawakukubali kuyumbishwa kwa namna yoyote ile kwenye hilo.
Waliamini wanakwenda kufanya makubwa mpaka jamii iliyowazunguka nayo ikawaamini kwenye hayo.
Kwa imani hiyo isiyoyumbishwa, waliweza kufanya makubwa sana.
Hilo pia ndilo unalohitaji ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Unapaswa kuanza kwa kuamini bila ya shaka yoyote kwamba una hatima kubwa ya maisha yako.
Jione ukiweza kufanya makubwa sana na yenye manufaa kwa wengine.
Amini sana kwenye hilo na usikubali kuyumbishwa na chochote kile.
Kile ambacho unakiamini sana bila ya kutetereka ndiyo kinakuja kuwa unabii wa maisha yako.
Anza kwa kuamini una hatima kubwa, jione ukiwa umezalisha matokeo makubwa kabisa na yenye manufaa kwa wengine.
Na pale wengine wanapokupinga au kukuonyesha haiwezekani, unawapuuza na kuzidi kuamini kwenye hiyo hatima yako.
Ni kupitia kuamini kwako kwenye hatima yako kubwa ndiyo wengine nao wanakuamini kwenye hilo.
Hilo litakupa kujiamini zaidi na kuendelea kufanya mambo makubwa.
Sheria ya leo; Una hatima ya kukamilisha mambo makubwa na kwa kufikiri na kuamini hivyo, unakwenda kutengeneza unabii binafsi ambao kwa imani kubwa unaweza kutimia.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji