#SheriaYaLeo (327/366); Pokea kila kinachokuja kwako.

Kwenye safari yako ya maisha, kuna mengi yatakuja kwako ambayo ni tofauti kabisa na mategemeo yako.

Kwenye hali kama hiyo ni rahisi sana kulalamika na kulaumu wengine kwa hayo unayokuwa unapitia.
Lakini kufanya hivyo hakutasaidia chochote.
Utaendelea kubaki kwenye hali hiyo hiyo.

Kitu pekee unachoweza kufanya ambacho kitakuwa na manufaa kwako ni kukubali na kupokea hali uliyokutana nayo.

Kufanya hivyo haimaanishi kwamba umekata tamaa. Bali unatumia vizuri nafasi hiyo kuhakikisha unafika kule unakotaka kufika.

Yaani unapokea hali yoyote unayokutana nayo, kisha kuigeuza kuwa njia ya kufika kule unakotaka kufika.

Kwa kuwa na mtazamo wa aina hii, hakuna kitu chochote kinachoweza kuwa kikwazo kwako.
Maana hata ukutane na ugumu kiasi gani, utaweza kuugeuza kuwa njia ya kuelekea kule unakotaka.

Ili uweze kutumia vizuri hali au nafasi yoyote unayokutana nayo, lazima kwanza uipokee, kisha uifanyie kazi kwa ubora wa hali ya juu.

Sheria ya leo; Pokea kila kikwazo kama sehemu ya kujifunza, kama njia ya kuwa imara zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji