#SheriaYaLeo (328/366); Sifia ukuu wa watu.
Kusifia ni kinyume na wivu – tunatambua mafanikio ya watu na kuyafurahia bila ya kujisikia vibaya.
Tunakubali ubora wao kwenye sanaa au sayansi au biashara bila ya kupata maumivu.
Hilo linaenda zaidi, katika kutambua ukuu wa wengine, tunasherekea uwezo wa juu kabisa wa jamii yetu wanadamu.
Tunashiriki na kujivunia mafanikio makubwa ambayo sisi binadamu tumeweza kuyapiga.
Kuwakubali huko wale waliofanya makubwa, kunatuinua kutoka kwenye mambo madogo madogo ya kila siku na kutupa utulivu mkubwa.
Sheria ya leo; Ni rahisi kuwasifia wale ambao tayari wameshakufa na wengi hufanya hivyo, kwa sababu siyo rahisi kumwonea wivu aliyekufa. Lakini unapaswa kuwasifia na walio hai, ambao wamefanya makubwa, ambao pia unaweza kuwatumia kama watu wa mfano kwako kujifunza kwao ili na wewe ufanye makubwa.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji