#SheriaYaLeo (331/366); Kuona unachotaka kuona.
Huwa tunapenda kuthibitisha mawazo ambayo tunayo, kwa kuonyesha kwamba ni sahihi.
Hivyo tunajikuta tukitafuta ushahidi wa kuonyesha hilo.
Tatizo linalokuja ni kwamba, ushahidi tunapata hauwi kweli, bali unakuwa ni upendeleo wa kile tunachotaka.
Inapokuja kwenye kuthibitisha mawazo tuliyonayo, huwa tunaishia kuwa na upendeleo. Tunajikuta tukileta ushahidi wa kupendelea kile tunachotaka.
Kwa njia hiyo, hatuoni ukweli, bali kile tunachotaka kuona.
Hivyo tunakuwa tunajidanganya sana sisi wenyewe.
Ili uweze kujua ukweli wa jambo lolote lile, usiangalie kile unachotaka kuona, badala yake angalia uhalisia uliopo. Ona kitu kama kilivyo na tafuta ushahidi wa kweli, siyo kile unachotaka kuona.
Hili siyo rahisi, hivyo lazima uanze ukiwa na wasiwasi kwako mwenyewe, kwamba mengi unayoamini na kuthibitisha, siyo ukweli, bali umeona kile ulichotaka kuona.
Sheria ya leo; Msukumo wako mkuu unapaswa kuwa ni kutafuta ushahidi unaothibitisha kile ulichoamini kwa muda mrefu siyo sahihi. Hiyo ndiyo sayansi ya kweli na inayokupeleka kwenye ukweli badala ya kujidanganya mwenyewe.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji