#SheriaYaLeo (332/366); Huwajui watu kama unavyodhani unawajua.

Hatari kubwa uliyonayo ni kudhani unaweza kuwajua na kuwaelewa vizuri watu kwa mwonekano wa haraka wa nje.
Watu wanaokuzunguka wamevaa sura ya kuigiza mbele yako, wakitaka waonekane kwa namna fulani, ambayo ni tofauti na uhalisia wao.
Kama utakuwa haraka kukimbilia kuamua, utaishia kuamua isivyo sahihi.

Unapaswa kwenda kinyume na mazoea yako ya kuhukumu watu haraka.
Anza kwa kujiambia huwajui watu kama unavyodhani unawajua.
Kubali kwamba inapokuja kwenye kufanya maamuzi, unasukumwa zaidi na hisia badala ya mantiki.
Na hayo ndiyo yamekuwa yanasababisha matatizo unayokutana nayo.

Fungua akili yako na uwaone watu kwenye mwanga mpya.
Usidhanie chochote kwa watu.
Chukulia kila mtu unayekutana naye nchi mpya ambayo bado haijajulikana. Yenye kila aina ya vitu ambavyo havijulikani.
Mara zote kuwa tayari kushangazwa na mambo ambayo hukutegemea kuyakuta kwa watu.

Sheria ya leo; Usiwe mgando na kutumia mazoea kuwahukumu watu kwa mwonekano wa nje. Badala yake jipe muda kuwaelewa watu kwa undani, ukijua kila mtu ni tofauti na ana mambo ambayo huwezi kuyajua kwa haraka.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji