#SheriaYaLeo (335/366); Nenda mbele kwa kusudi.
Kwenye historia ya jeshi, kuna aina mbili za majeshi.
Aina ya kwanza ni jeshi linalopigana kwa kusudi kubwa. Jeshi hilo huwa tayari kupambana kwa kila aina na hata kufia katika mapambano.
Aina ya pili ni jeshi linalopigana kama sehemu ya kazi na kupata pesa.
Kwa jeshi linalopigana kwa kusudi, nguvu ya kupambana ni kubwa na msukumo wa kuendelea haupoi.
Nguvu hii inawaunganisha wapambanaji wote kwa pamoja na nguvu ya jumla inakuwa ni kubwa zaidi.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye maisha, kuna watu wanafanya kitu kwa kusudi na wanaofanya kama kazi au kutegemea kulipwa/kupata fedha.
Wanaoongozwa na kusudi huwa wanapambana kwa juhudi kubwa bila kukata tamaa na hilo linawapa ushindi mkubwa.
Wanaoongozwa na maslahi huwa wanakata tamaa haraka wanapokutana na magumu au changamoto.
Kama ambavyo kusudi linaleta pamoja jeshi, ndivyo pia linavyoleta pamoja nguvu zote zilizo ndani ya mwili wa mtu na kumwezesha kupambania kusudi lake.
Unapokuwa na kusudi kubwa, akili yako, nguvu zako, umakini wako na hata hisia zako, vyote vinaungana pamoja kukupa nguvu kubwa ya kulipambania kusudi hilo.
Unaweza kuvuka kila aina ya ugumu na kuweza kufanya makubwa.
Sheria ya leo; Kwenye ulimwengu ambao watu wengi wanazurura, wale wenye kusudi ndiyo wanaoweza kufanya makubwa. Jua kusudi lako likupe msukumo wa kufanya makubwa na kufanikiwa.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji