#SheriaYaLeo (345/366); Ona kwa ujumla.

Sisi binadamu huwa tuna tabia ya kuona vitu kwa utengano.
Tunajiona sisi na wengine kama watu binafsi na waliojitenga badala ya kujiona kama kitu kimoja ambacho kimeungana.

Huwa tunaiangalia dunia kwa utengano wa viumbe na vitu mbalimbali, badala ya kuangalia jinsi vyote vinavyokuwa vimeungana pamoja.

Viumbe na vitu vyote ambavyo vipo hapa ulimwenguni, tunaunganishwa na kuwa kitu kimoja.
Kile kinachotuunganisha kwa pamoja siyo rahisi kuonekana kwa macho.
Ni lazima ujifunze kufikiri na kuona kwa utofauti ndiyo uweze kuona jinsi tunavyounganishwa pamoja.

Unachopaswa kujua ni kwamba kuna ujumla ambao kila kitu kilichopo duniani kipo ndani yake.
Ujumla ambao unajumuisha kila kitu kikichopo ulimwengu na kuviunganisha kuwa kitu kimoja.

Ujumla huo ndiyo unaifanya dunia kwenda na kuzalisha matokeo ambayo yanaonekana.
Kwa kuiangalia dunia kwa ujumla huo, unajifunza na kuelewa mengi.

Sheria ya leo; Unapoiangalia dunia, acha kuviona vitu kwa utengano, badala yake ona vyote kwa ujumla na muunganiko wake. Ione dunia kama kitu kimoja ambacho kimekuwepo kwa mabilioni ya miaka, wewe ukiwa sehemu ndogo na muhimu kwenye hilo.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji