2843; Kuweka matumaini yako kwa wengine.

Kuweka matumaini yako kwa wengine ndiyo kitu ambacho kimekuwa kinakuangusha kila mara.

Huwa kuna usemi kwamba ndege anapotua kwenye tawi la mti, siyo kwa sababu anaamini tawi hilo ni imara, bali kwa sababu anaamini mabawa yake yanaweza kumrusha.

Kama ndege angetua kwenye tawi kwa kutegemea uimara wa tawi pekee, likivunjika angeumia.
Lakini kwa kuwa anaamini kwenye mabawa yake, tawi likivunjika anaweza kuruka.

Maamuzi yoyote unayofanya kwenye maisha yako, hakikisha unaweza kuyasimamia wewe mwenyewe hata pale unaowategemea wanaposhindwa.

Kuweka matumaini yako yote kwa wengine, bila ya kuwa na njia ya kuweza kusimama mwenyewe imepelekea wengi kushindwa kwenye mipango mikubwa wanayokuwa nayo.

Hii haimaanishi usiwaamini na kuwategemea watu, bali inamaanisha uwe na nguzo imara ya kuweza kuendelea kusimama hata pale wote uliowategemea na kuwatumaini wamekukwamisha.

Hatua ya kuchukua;
Kwa kila matumaini unayoweka kwa wengine, jenga msingi wa kuweza kuyasimamia mwenyewe hata pale wengine wanapokuangusha.
Kwa sababu watu watakuangusha kuliko unavyotegemea.

Tafakari;
Kutegemea wengine wakufanyie kitu ambacho wewe mwenyewe umeshindwa kujifanyia ni kujidanganya. Chochote unachotaka kutegemea kwa wengine, hakikisha unaweza kukijenga ndani yako kwanza.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed