#SheriaYaLeo (350/366); Kitambue kifo kwa vitendo.
Huwa tunakihofia kifo kwa sababu tunajiweka mbali nacho.
Imekuwa ikielezwa kwamba dawa ya hofu ni kufanya kile unachohofia.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye kifo, kama hutaki kukihofia, unapaswa kukitambua kifo kwa vitendo.
Kujenga hali inayokukumbusha kifo kila wakati kiasi kwamba hukihofii tena.
Moja ya njia za kufanya hivyo ni kuchukulia zoezi la kulala kama kifo.
Kila unapolala, jione kama ndiyo unakufa.
Pale unapoingia kwenye usingizi, ona kama ndiyo umefikia tamati ya maisha yako.
Zoezi hili siyo kujichuria kifo, bali kukufanya uyathamini maisha yako, kwa kujua unaweza kufa muda wowote.
Badala ya kukihofia kifo, unayaishi maisha yako kwa ukamilifu wake na kuwa tayari muda wowote kukikabili kifo.
Kuhofia kifo haina msaada wowote kwako.
Badala yake kitambue kifo kwa vitendo kwa kukikabili kila siku na hilo litakufanya uyathamini maisha yako.
Sheria ya leo; Tumia akili yako kujenga taswira ya kifo, kukitambua kwa vitendo na kuona jinsi unavyoweza kukutana nacho muda wowote. Tumia utambuzi huo kuyathamini zaidi maisha yako na kuishi kwa ukamilifu.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji