2847; Kukaa kati.

Dunia inaendeshwa kwa upacha, pande mbili zinazotofautiana.
Usiku na mchana. Jinsia ya kike na ya kiume. Juu na chini.
Hizo hali zinaeleweka na kutengana wazi.
Huwa hazina katikati.

Changamoto nyingi kwenye maisha yetu huwa zinatokana na kujaribu kukaa kati.
Kushindwa kujitoa kweli kwenye upande mmoja wa kitu.
Tunataka kupata kila upande na mwishowe tunakosa pande zote.

Ukitaka mafanikio na utulivu kwenye maisha, chagua upande na zama kamili kwenye upande huo.
Usijaribu kukaa kati au kutaka kuonekana tofauti, ingia mzima mzima.

Kila upande una mazuri na mabaya yake. Una faida na hasara zake.
Ni wewe kukubali yote ili kusonga mbele.
Kukaa kati, ukidhani utapata faida na kuepuka hasara ni kujidanganya, hicho kitu hakipo.

Chagua upande wako kisha kuwa na nidhamu kali ya kuamua na kufanya kwa msimamo. Mafanikio yapo kila mahali ambapo nidhamu na juhudi vinawekwa.

Hatua ya kuchukua;
Jichunguze leo kwenye safari yako ya mafanikio, je umejitoa mzima mzima au bado umejiweka katikati.
Hunufaiki na chochote kwa kukaa katikati, jitoe hasa au usijitoe kabisa.

Tafakari;
Muda na nguvu nyingi zinapotezwa na wengi wanaokaa katikati, wanaojaribu badala ya kufanya kweli. Wanajikuta wakihangaika na mengi na mwisho kushindwa kupata mafanikio makubwa. Wewe chagua moja kisha weka kila kitu chako hapo, halafu uone kama hutafanikiwa.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed