#SheriaYaLeo (352/366); Kuona kitu kwa mara ya mwisho.
Kama binadamu tungekuwa tunaishi milele, maisha yangepoteza maana. Ni ufupi wa maisha ndiyo unatufanya tuyathamini na kufanya yale yenye tija.
Lakini wakati mwingine huwa tunajisahau na kuzoea vitu, kwa kuona vipo muda wote.
Ili kuondoka kwenye mazoea haya na kuvithamini vitu, tunapaswa kuchukulia tunaviona kwa mara ya mwisho.
Chukulia kila unachokiona ni kwa mara ya mwisho, kwamba hutakuja kukiona tena. Kadhalika kwa watu wanaokuzunguka, chukulia unawaona kwa mara ya mwisho.
Hilo litafanya uthamini muda na uwepo wa watu au vitu hivyo kwenye maisha yako.
Utavipa uzito unaostahili na kuweza kunufaika navyo.
Sheria ya leo; Leo, chukulia kila kitu unakiona kwa mara ya mwisho. Hilo litafanya uvipe uzito na kuvithamini zaidi.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji