2851; Uwezo tayari upo, tofauti ni matumizi.

Unga wa ngano, unaweza kutengeneza mandazi, chapati, mkate, keki na vingine vingi.

Uwezo wote huo tayari upo ndani ya unga, ila matokeo ya mwisho yanategemea jinsi ambacho uwezo huo umetumiwa.

Kadhalika kwetu binadamu, chochote ambacho wanadamu wengine wameshaweza kufanya, hata wewe una uwezo wa kufanya.

Na hata yale ambayo bado hayajafanyika na wengine, bado uwezo wa kufanyika upo.
Tofauti pekee ni namna uwezo huo unatumiwa.

Wasiofanya makubwa wanakuwa hawatumii kabisa uwezo walionao, au wanautumia vibaya.

Wanaofanya makubwa wanatumia uwezo huo, tena kwa kiasi tu.

Hatua ya kuchukua;
Ni nini hasa unachotaka kwenye maisha yako? Uwezo wa kukipata tayari upo ndani yako. Ni wewe tu kufanyia kazi.

Tafakari;
Usidharau unga wa ngano uliopika mandazi badala ya mkate. Uwezo tayari upo, haujatumiwa tu.
Kadhalika usijidharau kwa sababu hujafanya makubwa, uwezo tayari unao, ni wewe kuufanyia kazi tu.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed