Rafiki yangu mpendwa,

Peter Thiel kwenye kitabu chake cha Zero To One ametushirikisha aina tatu za malengo ambayo watu wamekuwa wanajiwekea.

Aina hizo tatu ndiyo chanzo cha watu kuwa na furaha au kukosa furaha kulingana na aina ya malengo ambayo wamejiwekea. Na hata kufanikiwa au kushindwa kwa mtu, kunatokana na aina ya malengo anayoweka.

Hapa nakwenda kukushirikisha aina hizo tatu za malengo na kisha kukuonesha ni aina ipi unayopaswa kujiwekea ili uweze kupata mafanikio makubwa na furaha kwenye maisha yako.

Aina ya kwanza ni malengo rahisi kufikia, haya hayahitaji hata ujitume sana. Malengo hayo unayafikia bila ya kufanya chochote. Haya ndiyo aina ya malengo ambayo watu wamekuwa wanajiwekea, na wanayafikia kweli lakini hayawafanyi kuwa bora. Unafikiri kwa nini mtu anafanya kazi au biashara kwa miaka kumi na kipindi chote hicho hakuna kikubwa alichofanya? Kwa sababu lengo lake ni moja, kusogeza maisha, hivyo anayasogeza kweli, anakula na kuishi, hakuna kingine kikubwa anachofanya. Pia malengo mengine ya kupata vitu, mfano kujenga nyumba, kuwa na gari na vingine, ni malengo rahisi kwa sababu yeyote anaweza kuyafikia kulingana na anavyoendesha maisha yake.

Aina ya pili ni malengo ambayo ni magumu kufikia, haya ni yale yanayokutaka ujitume sana, utumie uwezo wa kipekee ulio ndani yako ili uweze kuyafikia. Ili kufikia malengo haya, lazima ujitume sana, lazima ubadili kabisa maisha yako na uache kufanya yale uliyozoea. Unapofikia malengo haya, unakuwa mtu bora zaidi ya ulivyokuwa kabla. Malengo ya aina hii siyo yale ya ubinafsi, bali yanayokuwa na mchango mkubwa kwa wengine. Mfano wa malengo ya aina hii ni kuanzisha na kukuza biashara ambayo itatoa huduma bora kwa wengine pamoja na kuajiri watu wengi, hili siyo rahisi hata kidogo, linakutaka uwe mtu mpya kabisa. Malengo mengine yenye sifa hii ni yale ya kuleta mabadiliko makubwa kwako na dunia kwa ujumla, mfano kuja na njia bora ya kufanya kitu ambacho tayari kimezoeleka kufanyika kwa namna fulani, mfano mawasiliano, usafiri, matibabu n.k. Malengo magumu ndiyo yanayoleta maendeleo makubwa kwa watu na jamii kwa ujumla.

Aina ya tatu ni malengo ambayo hayawezi kufikiwa, haya ni yale ambayo huwezi kuyafikia kwa namna yoyote ile, hata ufanye nini. Malengo haya huwa yanaenda kinyume kabisa na sheria za asili na hakuna namna unaweza kuyafikia kwa usalama. Mfano wa malengo haya ni kutaka kupata matokeo makubwa bila ya kuchukua hatua yoyote, yaani kutegemea vitu vitokee vyenyewe tu. Hilo haliwezekani, haijalishi wewe ni nani, kanuni ya asili inategemea visababishi ili kitu kitokee.

Kwa nini watu hawafanikiwi na wanakosa furaha.

Watu hawafanikiwi na hawana furaha kwenye maisha yao kwa sababu malengo wanayojiwekea ni yale ambayo ni rahisi au ambayo hayawezekani. Wanapenda kuweka malengo haya kwa sababu hayawaumizi kwa namna yoyote ile, maana hayataki wajisukume zaidi ya walivyozoea.

Wanaweka malengo rahisi na wanapoyafikia wanaona hakuna cha tofauti sana, hivyo hawapigi hatua na pia hawapati furaha. Huwezi kufanya kazi au biashara miaka kumi na ukasema mafanikio yangu ni sijawahi kulala njaa na nimejenga nyumba na nina gari, hivyo ni vitu vya kawaida, ambavyo vinaweza kutokea tu hata ukiishi maisha ya kawaida.

Wakiweka malengo ambayo hayawezekani, hawayafikii na hapo wanajiambia wazi kwamba haikuwezekana. Hivyo hawapigi hatua lakini pia hawapati furaha, kwa sababu hakuna kilichobadilika.

Njia pekee ya kufanikiwa na kuwa na furaha, ni kuwa na malengo magumu ambayo unayafanyia kazi, yanakusukuma uwe bora zaidi na yanakutaka ubadilike kabisa. Kwa malengo ya aina hii, hata kama hutayafikia, hutabaki pale ulipokuwa, utakuwa bora zaidi kwa kuyafanyia kazi malengo hayo kuliko kutokuyafanyia kazi.

Karibu kwenye mazingira yatakayokusukuma uwe na malengo magumu.

Rafiki yangu mpendwa, umekuwa unajiwekea malengo rahisi au yasiyowezekana kwa sababu hicho ndiyo kitu ambacho jamii nzima inayokuzunguka inafanya.

Uliwaona wazazi wako wakipambana maisha yao yote ili kulisha familia, kupata nyumba ya kuishi na mahitaji mengine kama hayo. Hujawahi kumsikia mzazi wako akiongea mambo makubwa makubwa, bali ulimsikia akilalamika ugumu wa maisha na kwa namna gani amejitahidi kuwalisha, kuwasomesha na kuhakikisha mna maisha mazuri.

Umeingia kwenye kazi au biashara na umekuta wale waliopo kwenye kile unachofanya nao lengo lao ni kusukuma maisha tu. Wanachotaka ni hela ya kula, kulipa gharama mbalimbali za maisha na kufanya starehe wanazotaka. Hakuna yeyote mwenye mipango mikubwa ambayo inamtaka awe wa tofauti na kufanya tofauti.

Kwa mazingira ya aina hii, wewe mwenyewe unaona hakuna kingine kwenye haya maisha zaidi ya kufanya kazi, kula, kulipa gharama za maisha na kusubiri kufa.

Lakini mabilioni ya watu hapa duniani walifanya hivyo, na hakuna alama yoyote waliyoacha ambayo leo tunajivunia, wamepita hapa duniani kimya kimya licha ya kuwa na uwezo mkubwa ndani yao.

Hicho ni kitu ambacho sitaki kikutokee wewe rafiki yangu, hujaja hapa duniani kufanya kazi au biashara, ulipe bili mbalimbali za maisha na kisha ufe. Umekuja hapa duniani kuacha alama fulani. Lakini huwezi kuacha alama hiyo kama hujajua uwezo mkubwa ulio ndani yako na jinsi ya kuutumia.

Na ili kujua uwezo huo na kuweza kuutumia, unapaswa kuwa kwenye mazingira sahihi, yanayokuchochea wewe kufikiri tofauti na ulivyozoea kufikiri na kuchukua hatua za tofauti pia.

Mazingira hayo sahihi unayapata kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa kwenye KISIMA, unapata mafunzo, msingi, mwongozo na hamasa sahihi ya kuchukua hatua kwenye maisha yako ili upate mafanikio makubwa kwa chochote unachochagua kufanya. Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, unalazimika kujiwekea malengo makubwa na magumu, malengo yanayokusukuma sana ili uweze kuyafikia.

Lakini pia unapata mwongozo, hamasa na matumaini ya kuendelea kufanyia kazi malengo hayo licha ya magumu unayokuwa unayapitia kwenye maisha yako.

Karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo, ili na wewe uweze kujiwekea malengo makubwa na magumu, malengo ambayo yanakufanya uzaliwe upya na kutumia uwezo mkubwa uliopo ndani yako na kukufikisha kwenye mafanikio makubwa na furaha kwenye maisha yako.

Uzuri wa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni kwamba unazungukwa na wengine ambao nao wanapambana na malengo makubwa na magumu na kupiga hatua ili kufanikiwa zaidi kwenye maisha yao. Hivyo huwi mpweke, unakuwa kwenye jamii inayokuunga mkono kwa kile cha tofauti unachofanya.

Kwenye jamii ya kawaida ukiwa na malengo makubwa sana watu wanakushangaa na kukuambia haiwezekani. Kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA ukiwa na malengo makubwa watu wanakusifu na kukupa moyo kwamba inawezekana.

Hivyo kipimo rahisi sana kwako kukifanya leo ili kujua kama umejiwekea malengo rahisi au magumu ni kuwaeleza wengine malengo unayofanyia kazi, wapi unajiona miaka 10 ijayo. Kama wengi watakuambia ni malengo mazuri, basi jua umepotea, maana yake hayo ni malengo rahisi. Lakini kama wengi watakuambia ni malengo magumu, hayawezekani na utashindwa, basi hapo jua upo kwenye njia sahihi.

Rafiki, karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu tusafiri pamoja kwenye safari hii ya kujiwekea malengo makubwa na kujisukuma sana kila siku ili kuweza kuyafikia, kuwa bora sisi wenyewe na kuwasaidia wengine kuwa bora pia.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania