#SheriaYaLeo (355/366); Jua yaliyo muhimu.
Tuna malengo ya kufikia, miradi ya kukamilisha na mahusiano ya kuboresha.
Chochote tunachofanya kwa wakati wowote ule kinaweza kuwa ndiyo kitu cha mwisho kwetu kufanya.
Hivyo tunapaswa kuhakikisha kila tunachofanya ndiyo kilicho muhimu zaidi na kuweka juhudi zetu zote kwenye kitu hicho.
Kwa utambuzi huu wa ukomo wa maisha yetu na mengi yanayotuzunguka, tunaweza kuweka vipaumbele sahihi vya yale yaliyo muhimu zaidi kwako kuzingatia.
Tutaweza kuyapuuza yale yasiyo muhimu lakini yanatupigia kelele na kujaribu kunasa umakini wetu.
Tunachotaka ni kupata kuridhika na yale muhimu tuliyoweza kukamilisha kwa muda mfupi tulionao hapa duniani.
Sheria ya leo; Ufupi wa maisha yako hapa duniani unapaswa kukufanya uwe na vipaumbele sahihi kwenye yale unayofanya. Fanya yaliyo muhimu pekee na siyo kuruhusu usumbufu ukuvuruge.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji