2853; Ipokee kila siku kwa upendo.

Upendo ndiyo nguvu kuu inayoiendesha dunia.
Upendo ndiyo imani kuu inayowaleta watu wote pamoja.
Upendo una nguvu kubwa ya kuleta mapinduzi kwenye maisha ya kila mtu.

Ili kufanikiwa, unapaswa kuipokea kila siku kwa upendo mkuu.
Unapaswa kuongozwa na upendo kila siku.

Upendo unapaswa kuanzia kwako mwenyewe, ujipende na kujikubali vile ulivyo.
Kisha unapaswa kuwapenda wale wanaokuzunguka ili uweze kushirikiana nao vyema.
Halafu unapaswa kupenda kila unachofanya ili uweze kukifanya vyema.

Bila upendo wa dhati kutoka ndani ya moyo wako, huwezi kujenga mafanikio makubwa na yatakayodumu.
Upendo haupaswi kuwepo tu wakati mambo yanakwenda vizuri, upendo unapaswa kuwepo wakati wote.

Hatua ya kuchukua;
Ongozwa na imani kuu ya upendo. Jipende na kujikubali wewe mwenyewe vile ulivyo. Wapende sana watu wote unaojihusisha nao. Na penda kila unachofanya. Bila upendo, huwezi kufanya makubwa.

Tafakari;
Dini ya kweli na msingi mkuu wa kiroho ni upendo. Kama huna upendo, mengine yote unayofanya ni kujifurahisha na kujidanganya tu. Ipokee kila siku kwa upendo na ongozwa na upendo mara zote.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed